Xiaomi 18 Pro kuja Mwezi ujao na screen nzima nyuma ya simu

Na Mwandishi wetu,

Dar es Salaam. 

Xiaomi imeamua kuendelea na wazo ambalo bado ni nadra kwenye simu za kisasa—skrini ya pili nyuma ya simu.

Kampuni hiyo imethibitisha kuwa mfululizo wa Xiaomi 18 Pro utazinduliwa nchini China mwezi huu.

Skrini hiyo imewekwa ndani ya sehemu ya kamera za nyuma, eneo ambalo kwa simu nyingi hutumika kwa kamera pekee.

Xiaomi imeonyesha teaser ya simu hiyo ikiwa na neno “Generating” kwenye skrini, ishara inayoweza kuhusishwa na matumizi mengi ya akili bandia (AI).

Teknolojia hiyo ilianza kuonekana kwenye Xiaomi 17 Pro, ambapo watumiaji kuangalia saa, taarifa, muziki, wallpapers na baadhi ya huduma nyingine bila kutumia screen kuu.

Kwa mujibu wa Xiaomi, skrini hiyo ya nyuma kwenye 17 Pro ilipata zaidi ya mwingiliano milioni nne kwa siku kutoka kwa watumiaji huku zaidi ya wallpapers milioni 3.5 ziliwekwa kila siku.

Sababu hio pekee na zingine, zimeipa Xiaomi sababu ya kuendelea kuwekeza kwenye teknolojia hiyo ili idumu kwa generation hii na zinazokuja.

Hata hivyo, Xiaomi bado haijaeleza kwa kina features mpya zitakazopatikana kwenye toleo la 18 Pro.

Kinachojulikana ni kwamba matumizi ya AI inaweza kuwa sehemu muhimu na kubwa zaidi, na kupewa kipaumbele 

Hata Bei, vipimo kamili na taarifa kuhusu kuingia katika masoko mengine bado hazijawekwa wazi.

Xiaomi 18 Pro inaonesha kutamba na tech hii mpya, huku wengine akina iPhone, wakionesha kuvutiwa navyo.