Arsenal washabeba Ubingwa, sasa wanapata nini?


Na Charles Mkoka

Arsenal wamehitimisha rasmi ukame wa miaka 22 bila ubingwa wa Premier League na sasa wanajiandaa kupokea zawadi mbalimbali baada ya kutwaa taji hilo.

Arsenal watakabidhiwa kombe rasmi la Premier League Jumapili baada ya mchezo wao dhidi ya Crystal Palace katika dimba la Selhurst Park.

Kombe hilo lina uzito wa zaidi ya kilo 25 na hupambwa kwa utepe wa rangi za bingwa, na kwa Arsenal ni nyekundu na nyeupe.

Mbali na kombe, klabu hiyo pia itapata medali 40 za ubingwa zitakazotolewa kwa wachezaji, benchi la ufundi pamoja na viongozi wa timu.

Wachezaji waliocheza angalau mechi tano za ligi msimu huu wanastahili kupata medali hizo, akiwemo Bukayo Saka, Declan Rice, Martin Odegaard na William Saliba.

Kwa upande wa fedha, bingwa wa Premier League hapewi “bonus” maalum moja kwa moja, lakini hupata mgao mkubwa zaidi wa fedha kutoka kwenye ligi kwa kushika nafasi ya kwanza.

Msimu uliopita, bingwa alipata zaidi ya Tshs trilioni 180 kupitia mfumo wa malipo ya ligi.

Kila nafasi kwenye msimamo wa ligi huwa na thamani ya takribani Tshs bilioni 9 zaidi ya inayofuata.

Ubingwa huo pia unaipa Arsenal tiketi ya moja kwa moja kushiriki klabu bingwa ulaya (UEFA Champions League) msimu ujao, na huko ni kujizoela mkwanja mrefu zaidi kupitia matangazo, wadhamini na mapato ya mechi.

Mbali na fedha za ligi, ubingwa huo unaweza kuongeza mauzo ya jezi, thamani ya udhamini pamoja na nguvu ya kibiashara ya Arsenal duniani.

Soma