Canada Yashusha Leopard Tanks Lativia, Nato Yaongeza Presha Ulaya Mashariki

 Canada na washirika wake wa NATO wameendelea kufanya mazoezi makubwa ya kijeshi nchini Latvia huku mizinga ya kisasa aina ya Leopard 2 ikionekana kwenye operesheni mbalimbali za kivita.

Mazoezi hayo yamefanyika katika kambi ya kijeshi ya Ä€daži karibu na upande wa mashariki wa NATO. 

Vikosi kutoka Canada, Ufaransa, Poland, Sweden na mataifa mengine ya NATO vilishiriki.

Wanajeshi wa infantry walifanya mazoezi ya kusonga vitani huku wakilindwa na Leopard 2 tanks zinazotajwa kuwa miongoni mwa mizinga yenye nguvu zaidi duniani.

Kulikuwa pia na mazoezi halisi ya silaha za moto, mpangilio halisi wa kupambana vitani, na mazoezi ya mapigano ya mazingira halisi ya vita kwa msaada wa akili unde.

NATO imesema mazoezi hayo yanalenga kuongeza utayari wa kombat na kuhakikisha vikosi vya washirika vinaweza kufanya operesheni za pamoja kwa haraka wakati wa dharura.

Canada imeendelea kuwa moja ya nchi zinazoongoza vikosi vya NATO nchini Latvia kupitia operesheni ya “Operation REASSURANCE”. 

Mwaka 2023, Canada ilitangaza rasmi kupeleka Leopard 2 tanks Latvia kama sehemu ya kuongeza ulinzi wa NATO karibu na Russia.

Mazoezi hayo yanakuja huku mvutano wa kiusalama Ulaya Mashariki ukiendelea tangu kuanza kwa vita vya Ukraine.

Kwa sasa Latvia imekuwa moja ya maeneo muhimu zaidi ya NATO barani Ulaya kutokana na ukaribu wake na Russia na Belarus.

Soma