Akiupokea ujumbe huo wa Mhe Sam Nujoma Gavana wa Mkoa wa Khomas akiwa ameambatana na Mr Titus Shikongo Balozi wa Namibia Tanzania pamoja na Matheus Olavi msaidizi wa Gavana Mkuu wa Mkoa alipata wasaa wa kufanya mazungumzo wakijadili fursa mbalimbali zilizoko Mkoa wa Khomas Namibia na Dar es Salaam.
Aidha Gavana na wenzake waliweza kutembelea Bandari ya Dar es Salaam, SGR, na Makumbusho ya Taifa ambapo aliweza kujionea shughuli za kiuchumi zinazoendelea na historia ya Afrika hususani harakati za mapambano ya kulikomboa bara la Afrika.
Mwisho Gavana huyo bado yuko katika Mkoa wa Dar es Salaam ambapo anatarajia kuendelea kutembelea maeneo mengine ya Mkoa huo.
