Fedha hizo ni mkopo nafuu kutoka World Bank kupitia mfuko wa dharura wa CERC baada ya miundombinu mingi kuharibiwa na mvua za El-Nino mwaka 2024.
Mtendaji Mkuu wa TARURA, Victor Seff amesema miradi hiyo inaendelea kutekelezwa nchi nzima huku wastani wa utekelezaji ukifikia asilimia 70.
“Kazi zote zinatarajiwa kukamilika ifikapo Septemba 2026,” amesema.
Akizungumza akiwa kwenye ziara ya mradi wa daraja la mita 22 pamoja na barabara za maingilio katika Manispaa ya Tabora, amesema tathmini ya Serikali ilibaini maeneo mengi yaliharibiwa na hivyo kuhitaji matengenezo ya haraka ili kurejesha huduma za usafiri na mawasiliano.Amesema miradi hiyo pia imekuwa fursa kwa makandarasi wazawa ambao wanaendelea kushiriki kwenye utekelezaji wa kazi mbalimbali za miundombinu.
Kwa upande wake, Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya TARURA, Nunu Mangu amesema daraja na barabara zinazojengwa zitasaidia wananchi kupata usafiri wa uhakika katika misimu yote ya mwaka.
Aidha, amewataka wananchi kuitunza miundombinu hiyo huku Serikali ikiendelea kuwekeza fedha nyingi kuboresha sekta ya usafiri nchini.

