-Asisitiza utoaji wa huduma bora kwa wananchi
-Ataka changamoto zilizopo kutatuliwa mara Moja kwa maslahi mapana ya wananchi
-Aagiza uwasilishwaji wa taarifa mapema kwa sektetarieti ya Mkoa sambamba na upangaji wa tarehe ya vikao hivyo
Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam Ndg. Abdul R. Mhinte amezitaka Taasisi na Mamlaka za Serikali za Mitaa katika Mkoa huo kuhakikisha Kila wanapokuwa na vikao katika maeneo yao ya kazi suala la AFCON 2027 lijadiliwe ili kupanga namna ya kulifanikisha suala hilo kisekta
RAS Mhinte ameyasema hayo katika kikao Cha Robo ya Tatu ya Mwaka 2025/2026 cha Sektetarieti ya Mkoa na Taasisi za Umma kilichofanyika tarehe 2 Juni, 2026 na kile Cha Sektetarieti ya Mkoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kilichofanyika tarehe 3 Juni, 2026 katika ukumbi wa Shamba Hall uliopo maeneo ya Shangwe Kibada katika Manispaa ya Kigamboni
Hata hivyo Katibu Tawala huyo amesisistiza utoaji wa huduma bora kwa wananchi kwani ndio lengo hasa la kikao hicho na kupelekea kufanya Mkoa wa Dar es Salaam kuwa Salama
Aidhaa, RAS Mhinte amezitaka changamoto zilizopo kutatuliwa mara Moja kwa maslahi mapana ya wananchi ambapo aliyataja mambo kama ya migogoro ya Ardhi, uwepo wa Foleni, changamoto ya mfumo wa upatikanaji wa tiketi za SGR, uwepo wa makontena jangwani, uvamizi wa maeneo ya wazi ni mojawapo ya changamoto zinazopaswa kutatuliwa na kutoa majibu chanya kwa wananchi
Vile vile Katibu Tawala ameagiza uwasilishwaji wa taarifa kwa Sektetarieti ya Mkoa mapema ili sektetarieti iweze kuzipitia na kufanya masahihisho inapohitajika sambamba na kupangwa tarehe ya vikao hivyo mapema ili kuwawezesha Wajumbe kufahamu muda na eneo la kikaoKwa upande wao Wakurugenzi wa Mamla za Serikali za Mitaa, Viongozi wa Taasisi mbalimbali katika Mkoa wa Dar es Salaam wamepongeza uwepo wa vikao hivyo kwani vinafanya Mawasiliano yao kuwa karibu na kurahisisha utendaji wao wa kazi unaopelekea kutoa huduma bora kwa wananchi

