ChatGPT ya nne tovuti zinazotembelewa zaidi duniani

NB: Picha hii imetengenezwa kwa msaada wa akili unde (AI)

Na Charles Mkoka

Ikiwa una-Google, au unacheki YouTube, na unashinda au kuchungulia kwenye mitandao ya kijamii ujue wewe ni mmojawapo wa unaoewezesha takwimu ya mamia ya mabilioni ya watembeleaji wa mitandao hiyo, kila mwezi.

Takwimu za hivi karibuni zinasema kwamba, majukwaa ya akili unde (AI) yanachukua nafasi kubwa katika matumizi ya intaneti duniani, ikizidiwa kiduchu tuu na google, Youtube na kuacha pia Facebook kwa kutazamwa mara 

Ripoti mpya ya Visual Capitalist, iliyotumia takwimu za Semrush za Septemba 2026, inaonyesha kuwa ChatGPT imekuwa tovuti ya nne inayotembelewa zaidi duniani, ikiwa na ziara bilioni 8.23 kwa mwezi, ambapo kwa Mwezi oktoba, huenda ikawa imeipita Facebook.

Katika orodha hiyo, Google inaongoza kwa kutembelewa mara bilioni 108.9, ikifuatiwa na YouTube yenye bilioni 59.97 na Facebook yenye bilioni 12.21. Instagram inashika nafasi ya tano kwa kutembelewa mara bilioni 6.81.

Matokeo hayo yanaonyesha namna matumizi ya AI yanavyozidi kukua na kukomaa katika shughuli za matumizi ya mitandao kwa ujumla, huku bei za vifaa vinavyotumia RAM na Graphics Cards (GPU) kupanda bei zaidi. 

Urahisi huu unasababishwa na matumizi ya kila siku katika kutafuta majibu ya hapa na pale, kujifunza, kufanya tafiti, kurahisisha kazi, kuandika na hata kupata msaada wa utambuzi wa haraka katika kazi au mambo mengine mbalimbali.

Mabadiliko hayo yana athari kwa Tanzania, kwani Takwimu za hivi karibuni za Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) zinaonyesha kuwa hadi Juni 2026, usajili wa huduma za intaneti ulifikia milioni 62.79, huku matumizi ya data yakiongezeka kwa asilimia 11.65 katika robo hiyo na kufikia petabyte 1,041.

Kwa Watanzania, ukuaji huu unaonesha jinsi tunavyotumia teknolojia katika elimu, biashara, kazi na huduma zingine nyingi. Sasa hivi, mjasiriamali anatumia AI kuandaa maudhui ya biashara yake, akirekodi mwenyewe na kujipost mitandaoni, akilipia matangazo aidha kwa META Ads au njia zinginezo, au wanafunzi wanaotumia muda mchache kujifunza kitu kilichofanyiwa tafiti kwa miongo kadhaa. 

Hata hivyo, watumiaji wanapaswa kuhakiki taarifa wanazopata, kulinda taarifa zao binafsi na kuepuka kutegemea majibu ya AI bila kuyathibitisha.