Bilionea tajiri zaidi Afrika, Aliko Dangote, ameibua mjadala mkubwa baada ya kuonekana kutaka kuwekeza mradi mkubwa wa mafuta Afrika Mashariki.Ripoti za kimataifa zinaeleza kuwa Tanzania na Kenya zote zinafukuzia uwekezaji huo ambao unaweza kubadili biashara ya mafuta kwenye ukanda huu.
Dangote tayari anamiliki refinery kubwa Nigeria yenye uwezo wa kuchakata mapipa 650,000 ya mafuta kwa siku.
Tanzania inatajwa kutumia nafasi ya Bandari ya Tanga pamoja na mradi wa bomba la mafuta la EACOP kuvutia deal hiyo, huku Kenya ikipewa nguvu na Bandari ya Mombasa pamoja na ukubwa wa soko lake la mafuta.
Wachambuzi wanaamini mradi huo unaweza kuongeza ajira, biashara na uwekezaji mkubwa kwenye sekta ya nishati Afrika Mashariki.
Kwa Tanzania, uwekezaji huo unaweza kuongeza umuhimu wa Bandari ya Tanga pamoja na miradi mingine ya mafuta na gesi inayotekelezwa nchini.
Dangote tayari ana uwekezaji Tanzania kupitia kiwanda chake cha saruji Mtwara, lakini huu unaweza kuwa moja ya deal zake kubwa zaidi kuwahi kuingia East Africa.