Infinix HOT 70 yatua na rangi zinazobadilika, betri kali na camera ya 50MP


Na mwandishi wetu,

Katika miaka ya karibuni, tofauti kati ya simu za gharama kubwa na zile za bajeti inandelea kupungua. Simu za bei chee haziji tena kwa ajili ya kupiga simu au kutuma meseji, zinakuja na muonekano wa kisasa, uwezo wa AI na teknolojia ambazo zamani zilionekana kuwa za 'bei mbaya'.

Infinix Hot 70 iliyotangazwaga tangu mwishoni mwa mwaka jana, hatimaye imezinduliwa mwezi Mei 2026.

wenyewe wanadai wamekaza kwenye muonekano tofauti, betri inayodumu muda mrefu na uwezo wa akili mnemba (AI).

Simu hii ina toleo la Thermo Orange, ambalo lina uwezo wa kubadilika rangi kulingana na joto la mwili au mazingira. 

Huko mitandaoni, Video mbalimbali za watu wakishika 'tambo' hilo na kuona mabadiliko ya rangi zimesambaa TikTok na Instagram, na kufanya zi trend.

HOT 70 ina kioo kikubwa cha inchi 6.78 chenye uwezo wa 120Hz, sawa tu na hot 60 series. tofauti yake kuu ni mwanga wa Active Halo Light unaozunguka eneo la kamera kwa ajili ya taarifa mbalimbali kama simu zinazoingia au hali ya chaji.


Toleo hili lina One-Tap AI Button, kitufe maalumu kinachoruhusu mtumiaji kufungua AI wake maalum ndani ya mguso mmoja.

HOT 70 inatumia processor ya MediaTek Helio G100 Ultimate inayolenga matumizi ya kila siku kama WhatsApp, TikTok, Instagram, YouTube pamoja na gaming ya kiwango cha kati. wadau wa gaming  wanasema simu hiyo imefanya poa kwenye PUBG na baadhi ya games za mission bila kupata joto, 

Ina betri ya 6,000mAh. Kama hauna mambo mengi, unaweza kutumia kwa siku nzima online, au hata siku mbili kama unaingia na kutoka. wana 45W Fast Charging pia, so, yah.

Kamera ni 50 MP na kwa wanaopost na kujiselfisha, inafanya vizuri kwenye mwanga wa kutosha Daylight ila kwenye mazingira yenye mwanga mdogo utahitaji usaidizi wa chanzo kingine cha mwanga kwa matokeo mazuri zaidi 

Kwa makadirio ya bei, naskia simu hii inasimama kati ya TShs 340,000/= hadi TShs. 410,000/=, na hii ni bajeti ambayo sio mbaya kwa wanaotaka simu za daraja la kati (midrange phones). 

siku hizi wanasema AI ndio kila kitu, wewe unaonaje?