Viongozi wa dini nchini kukutana dar kwa siku tatu

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Patrobas Katambi, amewakaribisha Watanzania, hususan viongozi wa jumuiya za kiraia, kuhudhuria mkutano utakaofanyika Mlimani City, Dar es Salaam, kuanzia Oktoba 28 hadi 30, 2026.

Amesema mkutano huo utajadili changamoto zinazokabili jumuiya za kiraia, kuimarisha ushirikiano kati ya jumuiya hizo, Serikali na jamii, pamoja na kupendekeza maboresho ya sera, sheria na taratibu zinazoweza kukwamisha utekelezaji wa majukumu yao.

Mkutano huo pia utajadili masuala ya haki, ustawi, amani, usalama na mshikamano wa taifa, huku Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, akitarajiwa kuwa mgeni rasmi.