Marekani, Brazil na Canada ndio “walishaji wakuu” wa dunia… Afrika bado nyuma kidogo
Kama dunia ingekuwa group project ya chakula, basi Marekani, Brazil na Canada ndio wale wanaobeba assignment yote huku wengine wakisindikiza kusapoti.
Ripoti mpya ya Visual Capitalist imeonyesha kuwa nchi 10 pekee zinachangia karibu nusu ya biashara yote ya chakula duniani
Marekani inaongoza kwa kuuza chakula nje ya nchi ikiwa na mauzo ya zaidi ya Tsh trilioni 470 kwa mwaka, ikifuatiwa na Brazil yenye zaidi ya Tsh trilioni 375. Canada, China, Mexico na Indonesia pia zipo juu kwenye list hiyo.
Cha kushangaza kidogo ni kwamba China, ambayo huzalisha chakula kingi sana, haipo juu kabisa kwenye exports kwa sababu wananchi wake wengi “wanakula wenyewe kwanza” kabla ya kuuza nje.
Kwa ukanda wetu, manaanisha wa Kiafrika, ni South Africa pekee ndio imeingia kwenye Top 30 ya dunia. Ndiyo. Bara zima. Nchi moja tu.
Wakati huo huo, nchi ndogo ya Netherlands inaendelea kushangaza dunia. Ingawa sio kubwa kwa ardhi, bado ni miongoni mwa wauzaji wakubwa wa chakula duniani kutokana na teknolojia ya hali ya juu ya kilimo, greenhouse farming na logistics nzuri na za uhakika.
Kwa kifupi, dunia ya leo haitegemei tu mashamba makubwa, bali inategemea technolojia, bandari, mnyororo wa thamani na uwezo wa kusafirisha chakula haraka duniani.
Na hapo ndipo nchi nyingi za ukanda wetu wa kiafrika bado tunapambana.
Ripoti hiyo pia imeonyesha kuwa migogoro ya kisiasa, gharama za mafuta na usafirishaji zimeifanya biashara ya chakula kuwa “silaha mpya ya uchumi.”
Nchi zinazoweza kulisha dunia sasa zina nguvu kubwa zaidi kwenye siasa na biashara za kimataifa.
Kwa Afrika Mashariki, wachambuzi wanasema eneo hili lina uwezo mkubwa wa kuwa food hub kutokana na ardhi, hali ya hewa na nguvu kazi kubwa ya vijana.
Lakini changamoto zetu ni bado zile zile; uhifadhi (maghala), usafirishaji, teknolojia ya kilimo, na upotevu mkubwa wa mazao baada ya mavuno.
Kwa Tanzania, tunaona serikali ikijitahidi kuwaongezea bajeti kila mwaka TARURA, na hii ili tuu kupunguza tatizo mojawapo la usafirishaji,
Dunia inalishwa na nchi chache sana, na hii inaleta tahadhari kama endapo ikitokea changamoto yoyote dhidi ya nchi hizo, huenda hali ikawa mbaya zaidi kwa maamuzi yaliyopo mezani kwao.
