GIGN: Kikosi Cha Siri Cha Ufaransa Kinachoweza Kuibuka Baharini Kimya Kimya

Kama umezoea kuona vikosi maalum kwenye filamu za Hollywood, basi kuna uwezekano mkubwa reality yake ipo karibu zaidi Ufaransa kuliko Netflix.

Picha zinazosambaa mtandaoni zinaonyesha wapiga mbizi wa kivita wa kikosi maalum cha GIGN wakiwa kwenye operesheni za majini zenye usiri mkubwa.

Hiki ni kikosi maalum cha polisi wa kijeshi nchini Ufaransa kinachojulikana kwa operesheni za kupambana na ugaidi, uokoaji wa mateka na misheni za hatari sana.

Lakini kilichovutia wengi zaidi si silaha zao pekee, bali ni namna wanavyoweza kuingia kwenye eneo la operesheni kupitia chini ya maji bila hata kutoa mapovu.

Makomando hao hutumia mfumo maalum wa kupumulia unaoitwa “closed-circuit rebreather”, teknolojia inayowasaidia kupumua chini ya maji bila kutoa hewa juu ya uso wa maji. Kwa lugha nyepesi, unaweza usijue kabisa kama wako karibu mpaka waibukie mbele yako.

Wakiwa wamevaa suti maalum nyeusi za majini na silaha fupi zenye vifaa vya kupunguza sauti, kikosi hicho hutumika kwenye operesheni za siri karibu na meli, bandari au maeneo ya pwani.

Commando Hubert, ambayo ni moja ya vikosi hatari zaidi vya jeshi la majini la Ufaransa, pia hushirikiana na GIGN kwenye misheni za kupambana na ugaidi wa majini na uokoaji wa mateka.

Kwa miaka ya hivi karibuni, vikosi vya aina hii vimeendelea kupata umaarufu mkubwa duniani kutokana na ongezeko la vitisho vya ugaidi, uharamia baharini na operesheni za siri za kimataifa.

Na ndiyo, ukiiona picha yao wakitokea baharini usiku huku hakuna hata bubble ya hewa juu ya maji… ujue hiyo si bongo movie. Ni kazi yao halisi.

soma

Pia soma