Goli La Scott Mctominary Latua Kwenye Noti Mpya Ya £20

Scotland imemuweka mchezaji McTominay kwenye notii ya fedha baada ya goli lake la “bicycle kick”

Overhead kick.

Mchezaji huyo wa zamani wa Manchester United McTominay amefurahia hatua hiyo iliofanywa na Benki kuu ya nchi yake, Scotland, ambayo iliifunga denmark hatua ya kuufuzu kombe la dunia.

Goli hilo la sarakasi liliwavutia wengi, kiasi cha benki kuamua kuliweka kwenye noti ya pauni 20 

Mashabiki wa soka Scotland wana sababu mpya ya kutabasamu baada ya goli maarufu la Scott McTominay kuwekwa kwenye noti mpya ya £20.

Noti hiyo mpya inaonyesha kiungo huyo akifunga goli la “overhead kick” lililowahi kusambaa sana mtandaoni na kwa mashabiki wa Scotland.

Mashabiki wengi wamesema kuwa hio ni moja ya heshima kubwa ambazo mchezaji anaweza kupata akiwa bado anaendelea kusakata kabumbu.

McTominay, ambaye amekuwa mmoja wa nyota muhimu wa timu ya taifa ya Scotland katika miaka ya karibuni, ameendelea kujijengea nafasi kubwa kwa mashabiki kutokana na magoli yake muhimu na kujitoa kwake uwanjani.

Scotland imekuwa ikitumia mara kadhaa matukio ya michezo na watu maarufu wa taifa hilo kwenye bidhaa za kumbukumbu na fedha maalum, lakini hatua hii imeonekana kuwa tofauti kwa sababu ya nguvu ya utamaduni wa mpira wa miguu kwa kizazi cha sasa.

Soma