Wajumbe wa mkutano wa Shirika la Forodha Duniani ukanda Mashariki na Kusini mwa Africa (WCO ESA) wakiongozwa na Katibu Mkuu wa Shirika la Forodha Duniani Bw. Ian Saunders wameipongeza Mamlaka ya Mwapato Tanzania (TRA) kwa maandalizi mazuri ya mkutano huo uliofanyika Zanzibar kuanzia tarehe 11 Mei 2026 hadi 16 Mei 2026.
Akizungumza wakati wa matembezi baada ya mkutano Bw. Saunders amesema Tanzania ni nchi nzuri sana na ina vivutio vingi vya utalii na hali ya hewa nzuri jambo ambalo limewafurahisha wajumbe wa mkutano huo uku akisifu ukarimu na huduma bora walizopata kipindi chote cha mkutano.
“Mkutano wetu Umeenda vizuri sana kwa sababu ya maandalizi mazuri na mazingira mazuri ya wenyeji wetu hapa Tanzania” amesema Bw. Saunders
Kwa upande wake Kamishna wa Forodha na Ushuru wa Bidhaa wa TRA Bw. Juma Bakari amewashukuru wajumbe wote wa mkutano huo kwa kuichagua Tanzania kuwa mwenyeji wa mkutano huo na kuwaomba isiwe Mara ya mwisho kuja Tanzania bali iwe chachu ya kuja Tanzania marakwamara.
“Tunawashukuru wajumbe wote wa mkutano huu kwa kuichagua Tanzania kuwa mwenyeji wa mkutano pia tunawakaribisha tena na tena kuja kutalii Tanzania” amesema Bw. Bakari
Mkutano wa WCO ESA umehitimishwa leo tarehe 16 Mei 2026 ambapo wajumbe wamepata nafasi ya kutembea maeneo kadhaa Zanzibar na kushuhudia mchezo wa kipekee wa Makachu eneo la Forodhani Zanzibar.
