Na Mwandishi wetu
Dar es Salaam. Wajumbe wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB) Julai 8, 2026 walitembelea Banda la Wakala wa Nishati Vijijini (REA) katika Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (Sabasaba).
Katika ziara hiyo, wajumbe hao walijionea teknolojia mbalimbali za nishati safi ya kupikia zinazohamasishwa na REA.
Baada ya kutembelea banda hilo, wajumbe walipata fursa ya kufurahia chakula kilichopikwa kwa kutumia majiko ya nishati safi ya kupikia.
Ziara hiyo ilikuwa sehemu ya shughuli za kutembelea mabanda na kujionea miradi pamoja na teknolojia zinazochochea matumizi ya nishati safi nchini.
REA inaendelea kutumia maonesho ya Sabasaba kutoa elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa nishati safi ya kupikia na mchango wake katika kulinda afya, mazingira na uchumi wa familia.