Na Mwandishi wetu
Dar es Salaam. Viongozi na wananchi mbalimbali wameendelea kutembelea Banda la Wakala wa Vipimo (WMA) katika Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (Sabasaba).
Katika siku ya 11 ya maonesho hayo, wageni wamepata fursa ya kujifunza kuhusu huduma za vipimo na umuhimu wake katika kulinda haki za watumiaji na wafanyabiashara.
Mbali na elimu, WMA imekuwa ikitoa zawadi mbalimbali zenye nembo na ujumbe wa wakala huo kwa wadau wanaotembelea banda hilo.
Wageni pia wanapata nafasi ya kuuliza maswali na kupata ufafanuzi kuhusu masuala ya vipimo katika biashara za kila siku.
WMA imewahimiza wananchi kutumia fursa ya maonesho hayo kutembelea banda lake na kujifunza zaidi kuhusu huduma zinazotolewa.
